Njia za ufugaji wa kuku
Kuna njia tatu ambazo zinatumika katika ufugaji wa kuku na wanyama wengine kama ngo’mbe na mbuzi. Kupitia makala hii leo tutajadili njia hizo kuu za uufugaji wa kuku
Njia za ufugaji wa kuku.
Ufugaji huria.
Hii ni njia ambayo inatumika na wafugaji wengi kijijini. Ufugaji huu unakuwa hauna gharama kubwa ya chakula kwani kuku wanakuwa wanajitafutia chakula wenyewe
Ufugaji huu unatakiwa uwe na eneo kubwa kwa ajili ya kuku kujitafutia chakula na pia ufugaji huu huria hauhitaji wafanya kazi wa kukuzaidia
Yaani wewe asubuhi una wafungulia kuku unawapa maji tuu chakula watajitafutia wenyewe.
Ufugaji huu maranyingi unakuwa na madhara makubwa ya kuku kuibiwa au kuliwa na vicheche. Pia ufugaji huu unasababisha kuku kupatwa na magonjwa kwani huwa wanasunguka sehemu tofauti tofauti na uko wanaweza kupata magonjwa hayo
Ufugaji wa nusu nnje nusu ndani.
Njia hii kuku wanatengenezewa fensi kubwa na ndani ya fenzi wanatengenezewa sehemu ya kulala yaani banda liñgine la kulala. Kuku mchana wanakaa nnje (ndani ya fenzi) usiku wanaingia ukouko kwenye banda ambalolimejengwa ndani ya fens.
Ndani ya fensi kunakuwa na vyombo vya kuwekea maji na chakula. Njia hii itazaidia kuondoa milipuko ya magonjwa, inazaidia kuongeza utagaji kwani kuku wanakuwa wanatafutiwa chakula na inazaidia kuondoa tatizo la wizi na kuku kuliwa na wanyama wa porini.
Kupitia njia hii utatakiwa ununue chakula na madawa kwaajili ya kusuiya milipuko ya magonjwa.
Pia njia hii inahitaji eneo dogo na liwe limejengewa fensi na banda la kulala.
Ufugaji wa ndani tuu.
Ufugaji huu ni mmzuri sana kama utakuwa umejipanga kwa chakula na chanjo .
Kuku wanakuwa wamejengewa banda moja ambalo linakuwa la kulala na kulia chakula na ndani ya banda kunatakiwa kuwe na mwanga wa kutosha na madirisha makubwa.
Kupitia njia hii kuku wanakuwa haraka kwani wanatafutiwa chakula na vitamini, pia njia hii nirahisi kumtambua kuku mgonjwa na inakuwa rahisi kumtibu kwani anapo onyesha dalili utamtenga na walio wazima..
Hakuna maoni: