tambua dalili na jinsi ya kutibu ugonjwa wa mufua ya kuku
Mafua ya kuku husababishwa na virusi ambao wapo wa aina tofauti kwa kuku, bata na ndege. Ugonjwa huu hujulikana kama mafua ya ndege au avian influeza kwa kingereza kwani kuna aina ya virusi ambavyo husababisha ugonjwa huu kwa ndege wa porini, kwa kuku ugonjwa huu huwapata kuku wa kubwa na wadogo kama unavyoona kwenye picha hii.
Dalili za mafua ya kuku.
Dalili za mafua ya kuku huanza kuonekana kuanzia siku ya kwanza mpaka siku ya saba. Dalili hutofautiana na umri wa kuku, aina ya kuku,na ukubwa wa kuku maranyingi kuku wa wiki moja hadi wiki nane wana vimba kichwa na sehemu za usoni huwa na uvimbe baadae kope za macho hugandamana pamoja na kutiririka makamasi japo kutiririka makamasi kunatokea kwa kuku wakubwa pia ugonjwa huu husababisha vifo kwa kuku wadogo ambao huathiriwa kwa kutoona na kushindwa kufikia chakula na maji maranyingi kuku wana dhohofika, wanapiga chafya,kutokwa na makamasi na machozi. Kuku ambao wanataga hupunguza utagaji kwa asilimia 90% na wakitaga mayai yanakuwa malaini. Pia kuku husinyaa na hushusha mabawa, kuku walio athirika na ugonjwa huu watasinyaa atakama hawatakufa.
Matibabu na jinsi ya kusuia
Tumia dawa aina zifuatazo kwa kufuata muongozo wa kwenye karatasi au kwenye kifungishio.
ANTIBIOTIC,SULPHEAMETHAZINE, OFULIDONE, FLUMEQUINE, FERAMYCINE na STREPTOMYCINE.
Ugonjwa huu husuiliwa kwa kutoa chanjo kwa kuku wadogo na wakubwa, pia kuku wagonjwa wanatakiwa kutengwa na kuku wazima, safisha nyumba na vyombo kwa dawa (disinfectant) kabla ya kuweka vifaranga au kuku wapya pia tumia matandiko yasiyo na vumbi. Imeakwa na mtaalam wako wa kilimo na mifugo Mr kavishe
Hakuna maoni: