njia bora ya kuanzisha ufuģaji wa kuku



Mpenzi msomaji leo napenda nikufundishe yale ambayo nina uzoefu nao kuhusu ufugaji wa kuku. Ndugu napenda nikujuze kuwa ufugaji wa kuku kumi na wawili unaweza kukuzalishia kuku mia mbili  kwa muda wa miezi mitatu. Kama ulikuwa unalifahamu hili karibu tena ujivunze mbinu nyingine za kukufanya wewe kuboresha zaidi na kama ulikuwa hufahamu leo ukisha jivunza naomba uchukue hatua ya kununua kuku mmoja mmoja kila wiki.
Napenda uanze na ufugaji wa kuku kumi na wawili, mitetea kumi na jogoo wawili ambao ni wakienyeji tena mitetea nunua ambao wako tayaru kwa kutaga na jogoo ambao wanawika, wape chakula cha mayai kila siku pamoja na mabaki ya chakula ndugu hao mitetea wakikaa wa muda wa wiki moja wa taanza kutaga tena wanapo taga hakikisha unawaandalia sehemu nnzuri ya kutagia ambayo haina unyevunyevu, na  hakikisha unakuwa makini na hao kuku kwa kuwapa chakula cha mayai kila siku  ndani ya siku kumi na tatu mpaka kumi na tano kuku wako watakuwa wamefikisha mayai kumi na tatu mpaka kumi na tano kwa kila kuku na watakuwa tayari kutamia.
Watakapo anzakutamia kwa kawaida hawawezi kuanza kwa siku moja wote lazima watapishana siku atakae anzakutamia utampa yai moja kwanza huku ukisubiria wengine waanze kutamia lengo ni kuwafanya kuku wako watamie kwa siku moja wote iliwatakapo angua iwerahisi kwako kuwalea vifaranga wote watakao anguliwa kwa wakati mmoja  watakapo anza kutamia lile yai moja ambalo umewawekea wale walio anza kutamia uliondoe na uwape  mengine kumi na matatu kwa kumi na mawili kwa kila mmoja. Kuku wako wakiwa wanatamia andaa sehemu nzuri ya kuwaweka vifaranga watakao anguliwa na kama utakuwa unauwezo wa kununua mayai au kupata mayai mengine yanunu ili kuku wako siku watakapo angua uwarudishie tena waendelee kutamia kwa siku nyingine ishirini na moja kwani kuku akiwa anatamia ukiwahi kuchukua vifaranga kabla hajatoka nnje na ukampa tena mayai huwa ataendelea tena kutamia kwa awamu nyingine.
Baada ya siku ishirini na moja utakuwa na vifaranga mia moja kama umewarudishia tena mayai baada ya siku  nyingine ishirini na moja utakuwa tena na vifaranga wengine mia moja. Ndugu msomaji kumbuka kuwa kuku wakiw wanatamia huwa wanahitaji chakula kwa wingi iliwaweze kutengeneza joto jingi kwa hiyo zingatia chakula pamoja na maji kwa kipindi chote cha kuku wakiwa wanatamia. Pia kuku kwa kawaida wanatakiwa watamie kwa awamu mbilituu yaani awamu yakwanza na ya pili.
Pia vifaranga walio anguliwa utatakiwa uwaandalie sehemu nzuri ambayo ina chanzo cha joto kama umeme taa ya chemli, jiko la mkaa au unaweza ukachemsha maji ukayaweka kenye dumu na ukayavunika vizuri na uka yaweka karibu na vifaranga, kwa vifaranga mia moja utatumia madumu manne ya lita kumi na uta chemsha maji marambili kwa usiku mmoja. Njia hii nirahisi sana na wala haina gharama kubwa zaidi ya kuchemsha maji tuu lakini unaweza ukatumia jiko au taa ya chemli kama utaweza kununua mufuta ya taa.

Hakuna maoni:

CHANGE LANGUAGE

Inaendeshwa na Blogger.