chakula cha nguruwe wadogo wanao kuwa



Vichanganyio vya chakula changuruwe wadogo wanao kuwa kilo 100.

Mahindi yaliyo sagwa kilo ishirini na sita, pumba ya mahindi kilo hamsini na mbili,mashudu ya alizeti kilo kumi na tano, dagaa walio sagwa kilo nne, chokaa ya mifugo kilo mbili, pig mix 0.5kg na chumvi 0.5 kg.
Hivyo ndio vichanganyio vya chakula cha nguruwe wa miezi mitatu mpaka wa miezi sita. Ndugu mfugaji kumbuka kuwa unapo wachanganyia nguruwe wako chakula hiki kwa nguruwe dume akifikisha miezi sita anakuwa na kilo sitini na kuendelea pia kwa nguruwe jike anapofikisha miezi sita anakuwa tayari kwa kupandikiziwa na dume.

Hakuna maoni:

CHANGE LANGUAGE

Inaendeshwa na Blogger.