MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KATIKA UANDAAJ WA VYAKULA VYA KUKU KWA KUTUMIA NJIA ASILIA

Image result for PUMBA KAMA CHAKULA CHA KUKU
Image result for VYAKULA VYA KUKU ASILI   Image result for MAHINDI KWA KUKU
Mfugaj bora anaweza akazingatia mabo yafuatayo katika uandaji wa vyakula vya kuku hususani kwa kutumia njia asilia
MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA
• Upatikanaji wa malighafi kama:- Mahindi mtama, pumba, nk. Kutegemeana na kinachopatikana katika eneo husika. • Uchaguzi wa malighafi utategemea uwezo wa mfugaji.
• Utengenezaji wa chakula unategemea rika la kuku unaowatengenezea.
• Kiasi au uwingi wa chakula kitakachotengenezwa kitategemea uwezo wa mfugaji kifedha.
• Mali ghafi zinazotumika kutengenezea chakula ziwe zimekauka vizuri ili kuepuka uwezekano wa kuota ukungu ambao ni hatari kwa afya ya kuku.
• Hata kama mali ghafi ni kavu ikaguliwe kuhakikisha kwamba haina ukungu na iwe haijaoza.

JINSI YA KUANDAA (MATAYARISHO).
• Andaa aina zote za viungo ghafi zilizo bora katika wingi wa kutosha (uzito).  Pumba au dona, mashudu n.k. viwe havikuvunda. Tena viwe safi yaani havikuchanganyika na uchafu wowote bila kushambuliwa na wadudu.
• Tayarisha kopo tupu lenye ujazo wa lita 1 kwa ajili ya kupimia.  Mfano wa kopo linalofaa ni lile la Pride, Kimbo au Blue band. Kila kiungo unachotaka kuchanganya pima ujazo wa lita moja ili ujue una uzito gani (waweza kuomba msaada maduka ya jirani wakupimie). Ukiishafahamu hivyo utaweza kupima uzito sahihi wa kuweka kwenye mchanganyika wako. Kwa mfano: Kama lita 1 ya pumba ni nusu kilo, ina maana mahali unapotakiwa kuweka kilo 1 utaweka lita 2 yaani makopo 2 ya lita 1.
 • Kama unaandaa kiasi kikubwa cha chakula ni vizuri uwe na mizani ya kutumia kwa ajili ya kuandaa chakula chenye uwiano sahihi. Maana ni rahisi kupoteza hesabu za makopo kama unaandaa chakula kingi. • Kama mchanganyiko wako wa chakula una dagaa, mahindi au mashudu hakikisha kwamba vitu hivi vinabarazwa mashineni kabla ya kuchanganya (yaani vinavunjwa vunjwa).
 • Baraza vyakula hivi upate chembechembe zinazolingana na rika ya kuku unaotaka kulisha chakula unachoandaa

Hakuna maoni:

CHANGE LANGUAGE

Inaendeshwa na Blogger.