MAFUA YA KUKU (infectious coryza) DALILI ZAKE NA MATIBABU YAKE KWA UJUMLA
Ni swali ambalo limeweza kuzua changamoto nyingi kwa wafugaji wengi kwa kutokuelewa ni nini maana ya ugonjwa wa mafua ya kuku.
Ugonjwa wa mafua ya kuku ni ugonjwa unaoitwa infectious coryza huenezwa na bacteria. anaeitwa (hemophilus paragallinarum). Ugonjwa huu hushambulia kuku aina zote. Na usipo kuwa makini kwenye usafi wa banda na vyombo , kuruhusu watu kuingia ovyo bandani au kuku wa jirani kuja kuingia kwenye banda lako; ugonjwa huu unaweza shambulia kuku wako kwa kila wiki.
DALILI ZA UGONJWA HUU
_Kuvimba uso chini na nyuma ya macho. _Kupumua kwa shida na kukoroma _Kutoka makamasi puani, _ Mdomoni kuwa na hali ya mterezo _Macho kuvimba
_Kushindwa kula. _Kupiga chafya , macho kuonekana kama yanatoka machozi
JINSI UGONJWA UNAVYOENEA:
_Ugonjwa huu huenea kutokana kuku mmoja kwenda kwa kuku mwingine, au kutoka banda moja kwenda banda lingine.
_Chanzo cha maambukizi ni maji na chakula kilicho chafuliwa na kinyesi cha kuku Mgonjwa. _Ugonjwa huu uneea na kuambukizwa kwa mfumo wa hewa pale kuku wanapopiga chafya.
NINI UNASHAURIWA UFANYE
Pindi ugonjwa unapo ingia bandani kwako wale kuku watakao onesha dalili za ugonjwa huu , watenge kisha wape tiba kuku wako wote; unatakiwa kuwatenga kwa ajili ya kupunguza maambukizi bandani.
DALILI ZA MZOGA UKIUPASUA
Usaha mweupe hadi njano huonekana kwenye macho na ndani ya pua
MATIBABU
Zipo dawa nyingi za kutibu ugonjwa huu antibiotic/ sulfa. Hizi ni baadhi tu.
Fluban Ganadexil Tylodox Teramycin.nk
Ushauri:Tumia fluban kwa Kuku wanaooneshadalili za mafua bila vifo.
Tumia Ganadexil/tylodox kwa Kuku wenye mafua ambao kuna vifo vimetokea.
Ufugaji mwema
by John Beneth
Johnbeneth54@mail.com
Hakuna maoni: