JUA BAADHI YA MAGONJWA YA KUKU YANAYOWEZA KUWAPATA MARA KWA MARA PAMOJA NA TIBA ZAKE
UTANGULIZI
Kuku kama wanyama wengine hushambuliwa
na magonjwa mbalimbali ambayo mengine
yanatibika kwa dawa na mengine hayana tiba
bali kuku hupewa chanjo maalumu ambayo
huzuia magonjwa hayo.Leo nitawaeleza baadhi
ya magonjwa ambayo hushambulia kuku mara
kwa mara na ambayo ni chanzo cha
kuwakatisha tamaa wafugaji wa kuku.
A.) MAGONJWA YANAYOHITAJI CHANJO
1> GUMBORO
Ugonjwa huu husababishwa na virusi.
DALILI ZA UGONJWA
-Kuku kuzubaa na kulundikana, pamoja na
kusinzia
-Kuku kuharisha
-Kuwa na vifo vingi kwa kuku
TIBA
Ugonjwa huu hauna tiba,,Kuku wakipewa Dawa
za oxytetracycline hupunguza vifo.
KINGA
wakinge kuku wapo kwa kuwapa chanjo ya
gumboro (Gumboro vaccine)
*2> MAHEPE (Marecks)*
Ugonjwa huu husababishwa na virusi*
*DALILI*
-Kuku hupata ulemavu na vifo vya mara kwa
mara.
*TIBA*
Ugonjwa huu hauna tiba
KINGA
Chanjo hutolewa kwa vifaranga wenye umri wa
siku moja,vifaranga hupewa chanjo ya mahepe
(Marecks vaccine)
3>NDUI YA KUKU (Fowl Pox)
Ugonjwa huu husababishwa na virusi.
*DALILI*
-Kuku hupatwa na vidonda kichwani.
-Kuku hupata uvimbe mweupe kwenye
mdomo na kushindwa kula.
TIBA
Ugonjwa huu hauna tiba.
KINGA
Chanja kuku wako wa siku 60-90 kwa chanjo ya
Ndui ya kuku (Fowl pox vaccine).
*4>MDONDO (New castle)*
Ugonjwa huu husababishwa na virusi
*DALILI*
-Ugonjwa huu hutokea kwa ghafla na kuenea
kwa haraka
-Vifo vya kuku huwa vingi
-kuku hupumua kwa shida
-Kuku hupooza na kulemaa miguu
-Kuku hupinda shingo yake
-Kuku hupunguza kutaga mayai
-kuku huarisha
-Kuku Kuzunguka zunguka na kutembea
kinyume nyume.
TIBA
Hauna tiba
*KINGA*
Chanja vifaranga wako na kuku wako kwa
chanjo ya Mdondo (New Castlef vaccine) na
urudie chanjo hii kila baada ya miezi mitatu.
*B.)MAGONJWA* YANAYOTIBIKA KWA DAWA
1>KUHARA DAMU (coccidiosis)(Koksidiosisi
Ugonjwa huu husababishwa na virusi.
*DALILI*
-Kuku huzubaa na kujikunyata
-Kuku kuharisha LinkedI chenye damu au
kinyesi cha kahawi
-Kuku hudhoofika,manyoya huvurugika na
kulegea mabawa na kuonekana kama wawevaa
koti
-Kuku hupungukiwa homa ya kula
-Vifo huwa vingi kwa vifaranga
*TIBA*
Wape kuku wako dawa kama Esb 3, Amprolium,
au Basulfa.
KINGA
Zingatia usafi wa banda la kuku na usiruhusu
unyevuunyevu katika banda la kuku,
*2>HOMA YA MATUMBO(Fowl typhoid)*
Husababishwa na bakteria
DALILI
-Kuku hupata homa kali
-Kuku huarisha kinyesi cha kijani au njano
-Vifo huwa vingi hasa kwa vifaranga wenye
wiki 1-2
-Kuku huzubaa,kuvimba viungo vya
miguu,kuchechemea,kukosa hamu ya kula
-Kuku wanaotaga hupunguza utagaji,hutaga
mayai yenye ganda laini na hupata vifo vya
ghafla
*TIBA*
Dawa za oxytetracycline kama
Furamax,Typhoprim hutibu ugonjwa huu.
KINGA
Hakikisha usafi wa banda na vyombo vya
chakula na maji kwa kuku.
Tenganisha kuku wagonjwa na wazima
C)MINYOO
Hushambulia kuku wote wakubwa na vifaranga
DALILI
-Kuku hukonda
-Kuku huarisha
-Kuku hukohoa
-Kuku hupunguza utagaji
-Kuku hudumaa katika ukuaji/hawakui vizuri
-Kuku hupungua uzito
*TIBA*
Tumia dawa za minyoo kama piperazine
KINGA
Wapewe dawa za minyoo mara kwa mara kila
baada ya miezi mitatu
D)VIROBOTO/CHAWA/UTITIRI
Hushambulia sana vifaranga na hutokea vifo
kwa wingi kwa vifaranga Kwa kuku wakubwa
tatizo halionekani kwa sana lakini nao
huathiriwa sana.
*DALILI*
-Kuku kutochangamka
-Ukuaji mdogo wa kuku
-Kuku kutotaga na kuhatamia vizuri kutokana
na kusumbuliwa na chawa,utitiri au viroboto
-Viroboto huonekana kuganda machoni
wakinyonya damu
TIBA
Tumia dawa za unga kama sevin dust
5% ,Malathion ,akheri powder kwa kuku wote na
mabanda yao.
KINGA
Boresha usafi wa mabanda ya kuku.
E)UKOSEFU WA VITAMINI A
huathiri sana kuku wadogo.
*DALILI*
-Kuku huvimba macho na kutoa uchafu mzito
kama sabuni ya kipande iliyolowana.
-Mara nyingi ugonjwa hujitokeza baada ya
kipindi kirefu cha kiangazi
TIBA
wape kuku wote dawa za vitamini za kuku
zinazouzwa dukani.
*KINGA*
Wape kuku wako mchicha na majani mabichi
mara kwa mara.
*ZINGATIO*
Fuata ushauri wa matumizi sahihi kwa kila
dawa pindi ununuapo katika duka la dawa..
Hakuna maoni: