FAHAMU YAFUATAYO KUHUSU MUHARO MWEUPE KWA KUKU DALILI ZAKE PAMOJA NA MATIBABU

Image result for uharo mweupe wa kuku

MUHARO MWEUPE (PULLORUM DISEASE): 
(Kuhara kinyesi cheupe)
Ni ugonjwa unao enezwa na bacteria (salmonella pullorum)
Mzunguuko wa maambukizi ya ugonjwa huu hupitia kwenye mayai ya kutotorewa hadi  kwa Vifaranga. Vifaranga huambukizwa kirahisi mnamo wiki 3 za mwanzo kwa kula chakula chenye bakteri wa ugonjwa huu.
    Dalili za ugonjwa kwa Vifaranga:
_Vifo vingi kutokea kwenye siku 10 za mwanzo _Kutokuwa na hamu ya kula _Vifaranga kuzubaa _Kulegea kwa mabawa na manyoya kuchachamaa _Kuvimba matumbo _Vifaranga kupiga kelele na kuzubaa huku wamefumba
macho _Kuharisha kinyesi cheupe /kinyesi kuganda kwenye sehemu ya kutolea  haja _Vifaranga kuchechemea na kuanguka kabla ya kufa 
Kupasua mzoga wa kifaranga:
1.Maini na mapafu kuvimba 2.Mapafu kupauka 3.Maini kuwa meusi mno 4. Moyo kuwa Si wakaida na kuwa na maji maji ya damu 5. Viungo vya miguu na vidole kuvimba. 
Dalili za ugonjwa kwa kuku.
_Vilemba au upanga kusinyaaa _Vifo kutokea Kati ya siku 4 au 5 _Manyoya kuchachamaa _Kuku kutoa uharo mweupe /unao nuka _Uzalishaji wa mayai kuwa chini sana.
Kupasua mzoga wa Kuku.
1. Mayai kwenye sehemu ya kizazi kuwa na rangi ya kijani kibichi /hadi weusi 2. Mfuko wa kizazi kujaa kiini cha njano cha mayai 3. Ini  kuvimba. 4. Uvimbe mdogo mdogo wa kijivu ulioenea kwenye misuri ya moyo
MATIBABU:
Tumia dawa yenye uwezo wa kuuwa bacteria kama Flume
Ebs3 Tremazine 30% Nk.
Ufugaji mwema
by John Beneth.. johnbeneth54@gmail.com

Hakuna maoni:

CHANGE LANGUAGE

Inaendeshwa na Blogger.