Kabla Ya Kuanza Kufuga Kuku Tambua Mbegu Bora Kwa Ajili Yako!
MBEGU BORA YA KUKU
Kabla hujaanzisha mradi wa ufugaji kuku, ni lazima utafute aina ya mbegu bora itakayo kuongezea kipato.
Kumbuka kuna aina nyingi za kuku na ni aina zuri zote. Ila kila mfugaji huwa na malengo sasa hayo malengo yako ndio yatakayo kufanya utambue ni aina gani ya kuku unaetakiwa kumfuga ili utimize malengo yako.
Kumbuka kabla hujaanza kufuga kitu cha kwanza Fanya uchunguzi sehemu ulipo ninini kina nunulika Zaidi.
Kwa mfano kama mayai yana soko Zaidi basi hapo unatakiwa ufuge kuku watakao kupatia mayai mengi , na kama nyama ya kuku inanunulika Zaidi Basi hapo unatakiwa ufuge kuku wenye sifa ya kukuwa kwa haraka , wenye maumbo makubwa na nyama nyingi.
Huo uchunguzi utakufanya wakati wa kuuza kuku au mayai usihangaike sana kuhusu soko.
SIFA ZA MBEGU BORA🌀
- Utoaji wa mayai kwa mwaka uwe mzuri
-Umbile la mwili na njisi aonekanavyo
-Uwezo wa kukua haraka
-Uwezo wa kuotesha manyoya haraka
-Uwezo Mkubwa mwilini wa kutengeneza chakula kuwa mayai au nyama
-Ulaji wa chakuka uwe mdogo ukilinganisha na uzalishaji wake
-Utagaji uwe wa muda mrefu kabla ya kupumzika
- Uwezo wa kuatamia na kuangua vifalanga wengi (Hii ni kwa kuku wa kienyeji)
FAIDA ZA MBEGU BORA🌀
Faida zipo nyingi hizi ni baadhi tu!!
👉Faida moja wapo ni kuwa mbegu bora ya kuku hukua kwa haraka , basi hiko kitendo cha kukuwa haraka kitakufanya wewe usitumie gharama nyingi kwenye kuwatunza; na hivyo utapata faida nyingi utakapo wauza
👉Faida ya pili ni wana muonekano mzuri kutokana na maumbo makubwa, hiyo itafanya wanunuzi kuvutiwa na kuku wako.
👉Kutokana na ukuwaji / utagaji bora itakuongezea kipato.
Hapa tutaona baadhi ya aina za kuku unazo weza kufuga.✅
Kuna aina nyingi ila hapa tutaona chache tu!!
1. KUROILER: 👆Aina Hii ya kuku ni zuri sana na hufugika katika mifumo yote , Huria, Ndani na Nusu huria. Pia kuroiler ni kuku wanao kuwa kwa haraka kama ukimpa matunzo bora kila mwezi anaongezeka kg 1. Japo wengi ni vigumu kufikia Hatua Hii ila itabaki kuwa mbegu bora na ubora wake utaonekana kama ukipata Vifaranga bora vya kuroiler ambao hawaja changanywa na kuku wa kienyeji. Pia hawa kuku wana soko katika pande Mbili
_Pande ya kwanza ni katika utagaji.
Hivyo kwa Mtu mwenye lengo la kufuga ili auze mayai ya chotara anaweza akafuga kuroiler
_Pande ya pili ni katika nyama
Kuroiler wana kuwa kwa haraka,wana taga, wana maumbo makubwa na nyama nyingi. Hivyo kwa Mtu anaetaka kufuga ili aje auze kuku pamoja na mayai aina Hii itamfaa
SASSO : 👆Hawa ni kuku wa kibiashara yaani ni broiler wa kienyeji. Wana kuwa kwa haraka sana miezi 3_4 sasso anakuwa yupo tayari kuingia sokoni kama akipewa matunzo mazuri. Wana taga Japo hawana historia zuri katika utagaji.
Kuku hawa kwa mwaka unaweza vuna Mara Tatu kwa makadrio ya miezi 4.
"Kwa mfano mwezi wa 1 ukiingiza Vifaranga bandani hadi mwezi 4 utawauza, mwezi wa 5 ukiingiza Vifaranga bandani hadi mwezi wa 8 utawauza , mwezi wa 9 ukiingiza Vifaranga bandani hadi mwezi wa 12 utawauza."
Kwahiyo ni mizunguuko 3 kwa mwaka mmoja.⚡
Huku kuku wa kienyeji pure mizunguuko 1_2 kwa mwaka⚡
BLACK AUSTRALORP (👆 Kuku wa Malawi).
Hawa ni kuku wazuri sana katika utagaji mayai wana taga mayai Zaidi ya kuroiler. Lakini kuku hawa hawana historia zuri katika kl ni wepesi hawana kl nyingi. Hivyo kwa Mtu anaetaka kufuga kuku kwaajili ya kuuza mayai wanafaa sana.
KUKU WA KIENYEJI PURE👇
Aina Hii ya kuku Hakuna asiye jua hali ya soko lake la mayai na nyama ni ya uhakika. Cha muhimu ni kuwafuga kibiashara, kuwafuga kwa malengo ili ukuaji wao, utagaji wao uwe mzuri.
✅Mimi sio muuzaji kuku hivyo ukiwa unahitaji Vifaranga vya kuku hao jaribu kutafuta, ila sio kwamba kuna uwezekano wa kuvipata kwangu
👉Kumbuka yote hayawezi timia pasipo matunzo bora. Chanjo, lishe bora, banda bora (usafi na matunzo kwa ujumla)
Kama hauna uzoefu katika ufugaji kuku ni lazima upate Mtu atakae kuelekeza au kusimamia mradi wako. Usijali hata kama itakukost pesa kidogo ni vizuri kitu cha muhimu ni maendeleo bora ya mradi wako
___________________________________________________________________________
Share link, like page yetu ya Fb ufugaji kwa maendeleo, comment
Hakuna maoni: