Mambo Yanayo Sababisha Kudumaa Kwa Miradi Ya Ufugaji Kuku Wa Asili




MAMBO YANAYO DUMAZA UFUGAJI KUKU/KUKU WA ASILI.



Ufugaji kuku hiki ni kama kipaji ambacho kama ukipenda kukiendeleza Basi utafanikiwa. Leo nasema na wafugaji kuku ambao hawapendi kukuendeleza kipaji chao lakini pia wanashangaa kwanini hawaoni mafanikio.

Katika ufugaji kuku kuna watu wanafuraha na sekta hiyo na Kuna wengine hawana hamu na sekta hiyo. Makundi haya ni ya watu tofauti na wenye mawazo tofauti !!

 Kuna baadhi ya wafugaji kuku wana tabia au mawazo ya kizamani namaanisha yaliopitwa na wakati ambayo huwa ni chanzo za kuchukia ufugaji Kuku.

Wengine hawapendi kufuga kuku wa kisasa au hybrid wakiogopa kuwa wanagharimu mno katika kuwatunza na mawazo yao huwapeleka moja kwa moja hadi kwa kuku wa kienyeji asili (pure breed) hawa wao ndio huwa wanazani ni kuku wasio kuwa na gharama katika kuwa Fuga.

Naandika kitu nilicho kutana nacho au nilicho hisi kuwa ni moja ya mawazo ambayo ni chanzo cha kudumaa ufugaji kuku wa asili. Yapo mengi ila haya ni machache tu .

1. KUWAZA KUWA KUKU WA KIENYEJI (ASILI) HAHITAJI CHANJO/DAWA

Magonjwa ni changamoto kwa kuku, kuku wako usipo wapa chanjo za magonjwa hatari kama mdonde, gumboro, ndui nk  na wakapatwa na ugonjwa  kuku wengi watakufa hiyo itasababisha mradi wako kuyumba na ni moja ya jambo linalo dumaza ufugaji kuku.

Kuwa makini na kuku wako kuwapa chanjo kama inavyo takiwa , pia kuwa makini na kuku wako pale wanapoumwa kuwapa dawa maalumu kwa ugonjwa huo ili kuku wako wapone haraka.

Fahamu kuwa kuku ni kama viumbe wengine hivyo kama mwili wake utakuwa na tatizo basi ukuaji na hata utagaji wa mayai utapungua.

Kumekuwa na maswali mengi!! Kuku wangu wame stop kutaga? Au kuku wangu wamedumaa? Kuku wangu wanaumwa? Kuku wangu wamepunguza kutaga?

Hayo ni maswali ila katika hayo maswali tambua kuwa kuna chanzo kinacho Fanya hayo yatokeee


👉📝✅Hivyo ukitaka kufuga kuku kwa amani zingatia usafi, banda bora, mbegu bora, lishe bora, chanjo/dawa.✅


2. KUWAZA KUWA KUKU WA KIENYEJI (ASILI) HAHITAJI CHAKULA BORA

Chakula bora ni muhimu kwa kuku na mawazo ya watu wengi ni kuwa kuku wa kienyeji , unapo amua kumfuga unaweza tegemea yeye mwenyewe ajitafutie chakula. Katika ufugaji kuku kuna gharimu sawa, pia kuna ushindani sokoni, na kwa kawaida unapo Fuga kuku kitu cha muhimu kitakacho kuletea faida wewe ni ukuaji wa kuku wako.

Sasa kama hutawapa chakula bora eti kwasababu ni kuku wa kienyeji, ni lazima pia utegemee ukuaji hasi kwa hao kuku.

Na kama ukuaji hasi ukitokea kwa kuku wako basi inamaana kuku wako watadumaa.

Hio itasababisha kuku wako kushambuliwa na magonjwa Mara kwa mara, itasababisha pia kutokupata soko au hata kama ukipata soko utauza kwa bei ya chini kwasababu kuku wako wamedumaa.

Hapo hutoona faida ya ufugaji kuku na itakuwa ni mwanzo wa kuchukia ufugaji na kusema  kuwa Hauna faida

👉📝✅Hivyo ni vyema kuwapa kuku wako lishe bora ili uone mafaniko na ukuaji ulio bora✅

3. KUWAZA KUWA KUKU WA KIENYEJI (ASILI ) HAFUGIKI KISASA

Watu wengi wanapo amua kufuga kuku wa kienyeji mawazo yao ni kuwa kuku hao hawahitaji matunzo kama ya kuku wengine.

Unapo Fuga kuku wa kienyeji mpe matunzo yote yanayo hitajika kwa Kuku ili uone matokea na ukuaji mzuri kwa kuku wako.

4. KUKU WA KIENYEJI (ASILI) KUMFUGA KIASILI

Hilo ni wazo la watu wengi sana , kumfuga kuku wa kienyeji katika mfumo wa kienyeji Zaidi.

 Kuku anapo toka nje wewe hujui, kuku anapo ingia wewe hujui, kuku anapo kunywa maji wewe hujui, kuku anapo kula wewe hujui.

 Furaha yako ni pale unapo ona wanatembea tembea uwanjani.

 Hapo hujihisi kuwa na wewe ni mfugaji kuku. Na hapo ndio wengi hupenda na kuwa penda kuku wa kienyeji asili kuwa ni kuku wanao fugika kirahisi.

Basi kwa mawazo hayo hata ukuaji wa kuku wako utakuwa ni wakiasili na utagaji nao utakuwa ni wa kienyeji Zaidi.

Kuitwa kuku wa kienyeji haimaanishi uendelee kuwafuga kama kipindi kile cha mababu na mabibi ambapo walifuga bila kuwapa matunzo maalumu.

Na kama ukiendelea na mfumo huo wa zamani kwa hali ya sasa usitegemee  kufuga kuku labda tu utaishi na kuku.



Faida Za Kuku Wa Asili✅

(1).  Ni chanzo cha kipato
(2).  Nyama ya kuku ni protein tosha
(3).   Kinyesi cha kuku ni mbolea
(4).   Maganda na manyoya ni  mapambo
(5). Niwavumilivu wa magonjwa
(6). Wana wigo mpana kibiashara

Mahitaji Muhimu Kwa Ufugaji Kuku Wa Asili.

(1)   Banda bora
(2)   Mahali pakupata huduma na ushauri
(3)   Mahali pakupata mbegu bora

Banda La Kuku Wa Asili

(a)  Nyumba iwe mahali penye Kivuli

(b)   Paa liwe Refu kuruhusu kuingia mtu mzima
(c)    Nyumba iwe na uwezo wa kupitisha hewa
(d)   Mlango uangalie Kaskazini kupingana na jua
(e)    Iwe na mlango madhubuti na kufuli kudhibiti vibaka.

Ndani Ya Nyumba Ya Kuku Kuweje?

(1)Vichanja vya kulala kuku wakati wa usiku
(2)Viota vya kutagia na kuatamia
(3) Weka bembee ndani ya nyumba ya kuku
(4)Dawa za huduma ya kwanza

Aina Za Nyumba Ya Kuku

(1)   Nyumba ya tope
(2)   Nyumba ya matofali ya udongo au kuchoma
(3)   Nyumba ya kuinuliwa.

Muhimu👉👉✅Kibanda cha kuku wagonjwa na wageni katika banda🌀

_________________________________________________________


Share link/ Comment like page yetu ya Facebook @ufugaji kwa maendeleo

By John Beneth
Whatsapp tu 0744874288

TEMBELEA BLOG HII KILA SIKU

Hakuna maoni:

CHANGE LANGUAGE

Inaendeshwa na Blogger.