Zingatia Haya Jinsi Ya Kulisha Kuku Wako
ZINGATIA HAYA JINSI YA KULISHA KUKU WAKO
Lishe kwa kuku ni kitu muhimu sana, pia katika gharama za kuwatunza kuku chakula ndio huwa kina gharama nyingi mpaka ufikie muda wa mavuno ya mradi wako.
Gharama ya chakula isikufanye kuku wako usiwape chakula bora, ni vema uwatunze kuku wako vizuri ili upate matokeo bora.
Vitu vya Muhimu katika ufugaji lishe bora ni kitu moja wapo!!
👉Kumbuka katika vyakula vya kuku kuna aina ya vyakula kutegemea na aina ya kuku na umri wake.
👉Kumbuka ni vema kujua idadi ya kg wanazo kula kuku wako kwa siku.
Kwa mfano kama wana kula kg 10 kwa siku Basi asubuhi utawapa kg 7 jioni utawapa kl 3 zilizo baki.
Kuwa ongezea chakula ni pale utakapo ona wamemaliza na Bado wanauhitaji.
👉 Kuku hatakiwi kula chakula mpaka akaacha, Yaani unampa chakula Leo kina baki mpaka kesho, kesho tena unamuongezea , kina baki mpaka kesho kutwa hapo ni rahisi sana chakula kuharibika na bacteria kuzaliana
👉Kwa Vifaranga ni vema kuwapa chakula kingi ila wale hadi usiku, hasa wale ambao wali kosa kula vizuri mchana Basi wanakula usiku.
Chakula kwaajili ya usiku utawawekea kidogo tu🌀
👉Vifaranga wa nyama broiler hawa usiwapimie chakula, waache wale kama wanavyo taka. Kwasababu hawa ni kuku wa muda mfupi ikitokea wakachelewa kutoka bandani Hii itakuwa ni hasara kwako
👉Pia kuna formula ambazo unaweza tumia kuchanganya chakula cha kuku wako mwenyewe na mambo ya kaenda sawa katika mradi wako. Katika formula hizi hakikisha unapata formula bora yenye historia bora kwa kuku
👉Ufugaji una faida lakini faida hiyo huwezi kuiona kama hutozingatia lishe bora, ukuwaji mzuri wa kuku unasababishwa na vitu vingi ila kimoja wapo ni lishe bora.
👉Hata kama kuku wako unawapa chanjo, utawatibu, ni mbegu bora katika utagaji au huko uliko wa nunua wana historia zuri. Lakini wakikosa lishe bora tu hivyo vyote ulivyo vifanya ni kazi bure.
👉Ukitaka uamini Hii , umuhimu wa lishe bora, nenda kanunue mtetea ulioanza kutaga sehemu yoyote ile, uwe na historia zuri ya utagaji kisha mlete bandani kwako usimpe virutubisho muhimu kwa kuku.
Hapo ndipo utakapo jua umuhimu wa lishe bora kwa kuku, kama ataendelea kutaga vile vile au laaa!! ???
Pia lishe bora inapunguza magonjwa nyemelezi kwa kuku🌀
Kuna maswali mengi kuhusu wafugaji na kuku wao, Mara kuku wangu ka punguza kutaga, kuku wangu wamedumaa, kuku wangu hawatagi nk. Kitu chamuhimu ni matunzo bora kwa kuku wenu wapatieni chanjo, watibu kwa haraka watakapo onesha dalili za kuumwa , tafuteni mbegu bora , banda bora usafi wa banda na matunzo kwa ujumla.
Maana kuku akipewa lishe bora, kisha akakosa chanjo/ tiba Hakuna ufugaji bora hapo.🌀
Kuku wetu tuwapende tusitegemee ufugaji , kuwaacha kuku wajitafutie wenyewe chakula🌀
Unakuta wafugaji wengine kuku anajitafutia chakula hadi maji! ⚡
Je unaweza thubutu kusema ufugaji kuku haulipi?⚡
Katika banda la kuku kunatakiwa kuwepo na vyombo vya chakula na vyombo vya maji, idadi ya vyombo hivi hutegemea na idadi ya kuku.
Lakini kwa kawaida vyombo vya chakula vinatakiwa viwe vingi kuliko vyomba vya maji🌀
Kuku unapo wapa chakula kuku wengi watakimbilia kwenye chakula na kama vyombo vikiwa vichache Basi inaweza sababisha wengine kupigwa na kukosa kula.
Hapo ndipo utakuta kuku wako wana tofautiana ukubwa, mwingine umbo kwa wa wiki , mwinge kama wa wiki 3 mwingine wa mwezi. Hii yote ni kwasababu katika kula kuna wengine wanakosa kula na hupigwa na wazao walio wazidi umbo.
Lakini kwenye kunywa maji sio kuku wote watakao kimbilia hapo , wataenda wachache wachache🌀
Kuna vitu muhimu sana vinavyo hitajika kwa kuku aina zote, awe kienyeji, kisasa au hybrid
1. Kuku Anahitaji maji
2. Kuku Anahitaji vyakula vya madini
3. Kuku Anahitaji vyakula vya protin
4. Kuku Anahitaji vitamin
5. Kuku Anahitaji vyakula vya wanga
Hivi ni virutubisho muhimu kwa kuku visivyo chagua aina ya kuku. Na kama kuku akikosa kimoja wapo basi jiandae kuona dalili isiyo ya kawaida kwa kuku wako.
Hivyo tuwe makini katika kuwatunza kuku wetu, tuwafanya kama marafiki zetu, ajira zetu , kwa kuwapatia matunzo bora ili kuendeleza mradi yetu katika ubora.Lishe bora ndani ya ufugaji bora
Hakuna maoni: