MAMBO MUHIMU YA KUFUATA NA KUZINGATIA PINDI UNAPOWAPATIA KUKU WAKO DAWA YA CHANJO


Kabla ya kufanya jambo lolote  ni muhimu kabla ya kutoa chanjo jiandae vizuri kwa kuhakikisha kwamba hakuna ugonjwa wa kuambukiza kuku ama vidonda vyovyote, nawa mikono yako kwa maji SAFI na SALAMA yasiyotiwa dawa au kemikali na wewe pia usinawe kwa kutumia dawa yoyote au kemikali +sabuni pia kwani nayo ipo kwenye kundi la kemikali maji yanayotakiwa hapa ni maji yaliyochemshwa_. 
Hakikisha vyombo vyako vya kutolea chanjo vimeoshwa kwa maji SAFI na SALAMA na usitume dawa au sabuni au kemikali yoyote ile kuoshea vyombo vyako, dawa wala kemikali hazitakiwi kwa sababu chanjo nyingi za kuku huwa ni virus vilivyo hai dhidi ya ugonjwa fulani hivyo hivi vitu huwa vinaua hao virus kwa hiyo vitamfikia kuku vikiwa vimeshakufa hivyo utakuwa hujatoa chanjo bali sumu_. 
Siku ya chanjo usiwape kuku maji kwa masaa 3-4 au wapatie pumba tupu bila maji lengo lake ni kuwafanya kuku wawe na kiu kwa muda mrefu ili waweze kunywa na kupata dose kubwa ya chanjo,
Chanjo itolewe ndani ya masaa 2,baada ya hapo imwagwe, maana ukizidisha muda inakuwa sumu
Zoezi lifanyike haraka ili kupunguza usumbufu na kuharibika kwa chanjo_. 
Tenganisha kuku waliochanjwa na wasiochanjwa_. 
Fuata utaratibu wa kuharibu vifaa vya chanjo na utaratibu mzuri ni kufukia au kuchoma_
Beba chanjo katika hali ya ubaridi, vinginevyo chanjo itaharibika_. 
Weka kumbukumbu za uchanjaji kwenye daftari lako la takrimu za ufugaji

MAMBO AMBAYO HUTAKIWI KUFANYA UNAPOCHANJA KUKU

•Kumwaga chanjo ovyo na kuchafua nguo ama mikono.
•Kuchanganya chanjo za aina mbili au zaidi. 
•Kutuma chanjo iliyopita muda wake. 
•Kutumia chanjo iliyobaki. 
•Kuchanja kuku waliopatiwa dawa. 
•Kuchanja zaidi ya chanjo moja kwa wakati iwapo hukuagizwa hivyo. 
•Epuka kuweka chanjo kwenye mwanga mkali na joto kali,ili kuepuka kuua chanjo. 
• Epuka kutoa chanjo kwa kuku wagonjwa itolewe kwa kuku wenye afya tu. 
•Epuka kusafisha vyombo ama kunawa kwa kutumia dawa wala kemikali. 
•Epuka kutumia maji machafu na ya moto, maji yachemshwe na kupoozwa, yachemshwe siku moja kabla ya kutoa chanjo.

CHANJO

Aina za Chanjo kulingana na umri wa kuku

Siku ya 1
MAREK'S /MAHEPE
Chanjo hii hupewa kifaranga wa siku 1mara tu ya kuanguliwa na kinga hudumu kwa maisha yake yote, mara nyingi hutolewa hatchery kwenye makampuni yanayototolesha vifaranga ingawa baadhi ya makampuni hudanganya wafugaji kuwa wamechanjwa wakati hawakuchanjwa ila kwa kujiridhisha zaidi na uwe na uhakika na vifaranga wako unaweza kuchanja mwenyewe, wasipochanjwa siku ya 1 basi unaweza kuwachanja siku ya 18.

Namna ya kuchanja
Ni chanjo ya sindano hivyo ni vyema achanje mtaalamu anayejua. 

Siku ya 7
NEWCASTLE +IB VACCINE 
IB Ni Infectious Bronchitis (chanjo ya mafua) Hii ni chanjo iliyo kwenye chupa 1 lakini ina kinga ya magonjwa 2 ndani yaani Newcastle na mafua. Hii huwa ipo ukiikosa basi utanunua kawaida yenye kinga 1 tu ya Newcastle.

Jinsi ya kuwapa: 
huchanganywa na maji.

Siku ya 14
GUMBORO
Kwa kuku wa kienyeji chanjo hii huwa si lazima kupewa kwani wao huwa  wanatotolewa wakiwa na kiasi cha hii kinga.

Jinsi ya kuwapa: 
huchanganywa na maji.

Siku ya 21

Rudia chanjo ya NEWCASTLE

Siku ya 28

Rudia chanjo ya  GUMBORO

Baada ya siku hizi 28 mwezi sasa utakuwa umekwisha na chanjo za awali utakuwa umezitimiza sasa zitafuata chanjo nyingine nazo ni hizi zifuatazo_:

Wiki ya 6

Chanjo ya Ndui /Fowl pox:

Namna ya kuwapa: 
Chanjo hii ni vyema ikatolewa na mtaalamu anayejua kwani ni ya kuchanganywa kwanza na kuchoma kwenye mbawa (wing web) na kitendo hichi hufanywa kwenye kivuli pasipo na joto kali kwani hivi navyo ni virus hai.

Wiki ya 8:

Chanjo ya typhoid.

Namna ya kutoa:
Hii nayo hutakiwa kutolewa na mtaalamu anayejua kwani nayo ni ya sindano huchomwa kwenye msuli

MUHIMU

Baada ya hapo chanjo muhimu na ambazo zinapatikana kwenye mazingira yetu ya kitanzania ni hizo
Chanjo za marudio:

  MWISHO KABISA: 
Unashauriwa  Kila baada ya miezi 3 ni muhimu kurudia zoezi zima la kuwapatia kuku zako dawa ya chanjo ya NEWCASTLE
    
Asante kwa kutumia muda wako kusoma nakala hii  na nikutakie ufugaji mwema.

     

Hakuna maoni:

CHANGE LANGUAGE

Inaendeshwa na Blogger.