UFUGAJI WA KULOIREL

Ndugu mfugaji na mfuatiliaji wa Nakala zetu za ufugaji, nikusalimu apo ulipo, leo nimeonelea nikulete somo linalohusiana na ufugaji wa koroiler

UTANGULIZI

Kuloirel ni kuku chotara ambae asiri yake ni nchini india, na imetokana na mchanganyiko wa  dume la broiler na jike aina ya Rhode island red au dume la white legham na jike la Rhode island red.
ni moja kati ya kuku wasio na gharama kubwa katika kuwafuga lakini pia wana faida kubwa.
na kwasasa ni moja kati ya mbegu ambayo inafanya vizuri sana katika nchi nyingi na kwa east africa kuku hao upendelewa sana Uganda, Tanzania pamoja na kenya


SIFA ZA KULOIREL
  • Ni aina ya kuku ambayo inatumika kwa kazi zote yani nyama pamoja na mayai (duo purpose breed)
  •  kuku mmoja anauwezo wa kutaga mayai 150 hamsini kwa mwaka ukilinganisha na kuku wengine hutoa 40- 50 kwa mwaka.
  • madume ya  kuloirel hua yana kilo 3.5  na jike ni kilo 2.5  ukilinganisha na kuku wengine dume hua na kilo 2.5 na jike ni kilo 1.5.
  • pia ni moja kati ya aina ambayo haipati magonjwa kirahisi (disease resistance)
  • napia hawana gharama sana katika kuwalisha kwa sababu wanauwezo pia wa kula chakula kama kuku wa kienyeji. 
             

BANDA 
Kama kuku wengine banda lazima liwe bora ili kuweza kupata kuku bora pamoja na mayai mengi ila pia kuku wa aina ya kuroiler sio lazima uwafungie ndani moja kwa moja unaweza kutengeneza sehem ambayo utawafungulia ili kuweza kujipatia chakula(semi intesive) tofauti na kuku wa kisasa.

ila usafi ni muhimu hivyo ni vyema kuzingatia hilo 

CHAKULA 
Chakula ni lazima kiwe bora ili kupata kuku bora pamoja na mayai ya kutosha.
  • jike mmoja anakadiliwa kula kilo 5-8 kabla ya kuanzan kutaga
  • na ni muhimu sana kwa mfugaji kujifunza jinsi ya kuchanganya chakula mwenyewe
  • kuanzia siku 1 hadi wiki 4 unatakiwa kuwapa chakula cha kuanzia (chick starter mash)
  • kuanzia wiki ya 4 hadi 8 unawapa chakula cha kukuzia (chick grower mash)
  • Kuanzia wiki ya kwanza ya kutaga hadi mwisho unatakiwa kuwapa chakula(layersmash)
  • inakadiliwa kua na drinker 15 na vyombo vya kuliwa 20 ukiwa na wastani wa kuku 1000.

Image result for KUKU WA KUROILER


NIKUKUMBUSHE KU LIKE PAGE KWA WEWE AMBAYE BADO HAUJA LIKE ILI UWEZE KUENDANA NASI VIZUR UWAPO FACEBOOK, NA PIA USISAHAU KU SHARE POST ZETU KWA MANUFAA YA WAFUGAJI WENGINE.ASANTEN




















Hakuna maoni:

CHANGE LANGUAGE

Inaendeshwa na Blogger.