Soma: jinsi ya kuzalisha kuku kwa gharama ndogo



njia za kupunguza gharama za uzalishaji wa kuku.
Usafi na sayansi ya magonjwa na kinga. Zingatia usafi wa banda la kuku, vyombo vya kulia chakula pamoja na maji, hii itazaidia kupunguza milipuko ya magonjwa ya kuku pamoja na kuku ondolea gharama ambazo ungetumia kununua dawa kwaajili ya matibabu
Tumia chombo maalu kwaajili ya kuwekea chakula cha kuku. Unapotumia chombo maalumu kwa ajili ya kuwekea chakula cha kuku unapunguza gharama za uzalishaji kwani pale kuku wanapo mwagamwaga chakula kutakufanya ununue chakula ambacho usinge takiwa kununua kama ungetumia chombo kizuri kwaajili ya chakula.
Ndugu msomaji pia kama wewe unafuga kuku wa nyama, unaweza tumia chanjo wiki mbili za mwanzoni pamoja na usafi wa kutosha, kwani kuku wa nyama ni kuku ambao wanaweza kukupatia faida kubwa kwa muda mfupi pia wanaweza kukupa hasara kubwa kwa muda mfupi
Tunza kumbukumbu. Kumbukumbu kama gharama za chakula, chanjo, idadi ya wanao taga, jumla ya  kuku wote angalau kila mwisho wa wiki. Hii itazaidia kurekebisha tatizo lolote pale linapo tokea na kuweza kugundua tatizo lolote linalo waathiri kuku pia pale unapo tunza kumbukumbu utaweza kujua gharama za uzalishaji wa kuku kwa kiwango kikubwa.
Ni mimi mshauri na mtaalamu wako wa ufugaji kwa maendeleo Dr John

Hakuna maoni:

CHANGE LANGUAGE

Inaendeshwa na Blogger.