KAMA UNATAKA BIASHARA YAKO KUENDELEA NA KUKUA BASI JIBU MASWALI HAYA...!!!! SOMA HAPA
Angalia uwezekano wa biashara yako kuendelea na kukua (jibu yafuatayo)
a. Utawafikiaje walengwa wa biashara yako (Ni kwa vipi walengwa wako watajua kuhusu bidhaa na huduma zako)?
b. Utasambazaje/ fikishaje bidhaa/huduma zako (Bidhaa zako zitafikaje kwa wauzaji wa rejareja au huduma zako zitafikaje kwenye maeneo uliyokusudia na maeneo hayo ni yapi)?
c. Nini makadirio yako ya wafanyakazi unaohitaji kwa miaka miwili ya kazi (wafanyakazi wangapi utahitaji mwaka wa kwanza, na wangapi utahitaji mwaka wa pili)?
d. Unahitaji ufanye nini ili biashara yako ipate faida na itachukua muda gani kuwa na faida?
e. Nini matarajio yako ya mapato na matumizi kwa miaka 4 ya kazi (ni mapato na matumizi kiasi gani katika mwaka wa kwanza, mwaka wa pili, wa tatu na wa nne)?
f. Unahitaji mtaji wa kiasi gani (kiasi gani cha fedha unachohitaji kuwekeza) katika mwaka wa kwanza,wa pili, wa tatu na wa nne ili kuendesha biashara yako?
g. Utawezaje kupata kiasi hicho cha mtaji? Je ni kwa kuanza kuweka akiba katika benki au kuomba mkopo na kwa gharama gani?. Je mchango wako katika mtaji ni kiasi gani? Je mradi wako unaweza ukabeba gharama zinazotakiwa kiundeshaji na bado ukazalisha faida?...
Hakuna maoni: