KABLA YAKUANZISHA BIASHARA KWANZA TAMTHMINI WAZO LAKO LA BIASHARA…!!! SOMA HAPA
Hatua muhimu za kuzingatia
1. Nyambulisha na uainishe mradi unaotaka kufanya kwa msingi wa wazo linalotekelezeka
2. Fursa ya biashara hutokana na yafuatayo;
a. Tathmini ya wazo lako la biashara.
b. Tathmini ya kina ya mahitaji ya soko ambalo biashara yako italenga.
c. Tathmini ya kina ya bidhaa zako na huduma zako.
d. Tathmini ya kina na jinsi bidhaa yako/huduma yako itakavyokidhi mahitaji ya soko ulilolenga
e. Fikiria na ufafanue walengwa/watumiaji wa bidhaa au huduma zako.
f. Tathimini taratibu za kisheria na kiutawala kuhusu biashara unayotaka kuanzisha.
3. Angalia ushindani uliopo sokoni (husisha yafuatayo)
a. Angalia na uorodheshe biashara nyingine zinazotoa huduma/bidhaa kama unazotaka kutoa wewe.
b. Angalia na ujiulize kama wapo washindani wengine wapya wanaotaka kuingia kwenye biashara hiyo hiyo unayokusudia.
c. Jiulize changamoto zilizopo na vikwazo vilivyopo (kisheria, kimtaji, au vinginevyo) vinavyoweza kuzuia biashara nyingine zinazofanana na biashara yako kuanzishwa.
d. Jiulize na uorodheshe upekee wa bidhaa/huduma zako (jiulize sababu za kumfanya mtu ahitaji bidhaa/huduma yako badala ya bidhaa/huduma nyingine zilizopo sokoni)
Hakuna maoni: