Jivunza: namna unavyoweza kutengeneza chakula chakula cha vifaranga wadogo wanao kuwa 《grower mash》100kg
chakula cha vifaranga wadogo wanao kuwa.
Ndugu msomaji wa mtandao huu wa kavshe leo kupitia makala hii napenda ufahamu mahitaji muhimu yanayo hitajika iliuweze kutengeneza chakula cha vifaranga wadogo ambao ni kuanzia wiki nne mpaka wiki ishirini, pia napenda ufahamu jinsi ambavyo utachanganya mchanganyo huo wa chakula.
mahitaji ya muhimu katika utengenezaji wa chakula cha vifaranga wadogo wanao kuwa.
ndugu mpezi iliuweze kutengeneza chakula cha vifaranga wadogo kg 100 ni muhimu uwe na vitu vifuatavyo:
Pumba ya mahindi 50kg
Mahindi ya kuparaza 10kg
Mashudu ya pamba au ya alizeti 10kg
Dagaa au soya 15kg
Unga wa mifupa 5kg
Chokaa ya mifugo 9 1/4 kg
Chumvi iliyo sagwa 1/2 kg
Layer primix 1/4 kg
Hayo ndio mahitaji ya muhimu katika kuandaa chakula cha vifafanga wadogo wanao kuwa.
jinsi ya kuchanganya.
Andaa sehemu nzuri ambayo haina uchavu au takataka za aina yoyote ile au unaweza kuandaa kitambaa cha mvuko wa salvet kikubwa kiasi ambacho kitakuwa na mita mbili urefu na upana, pia unaweza ukachanganya kwenye baraza ya nyumba (kama ina sakafu) ndo nzuri ya kuandalia kwa ajili ya kuchanganyia.
Baada ya kuandaa sehemu yako ambayo umeichagua kwa ajili ya kuchanganyia chakula chako utafanya kama ifuatavyo.
Chukua pumba yako ya mahindi ambayo imepimwa vizuri kilogramu 50 anza kuiweka katika sehemu yako uliyo iandaa kwaajili ya kuchanganyia chakula chako.
Baada kuweka pumba weka tena juu yake mashudu ya alizeti au ya pambaa ambayo ni kilogram 10 ambazo umepima bila kupunguza au kuzidisha kwani kuzidisha au kupunguza itawafanya vifaranga wako wadumae.
Baada ya yakuweka mashudu utaweka mahindi yako yakuparaza kama ulivyo ya andaa kilogram 10 .
Ndugu ukishaweka mahindi ya kuparaza utaendelea kuweka dagaa ambao ni wale walio tolewa kwa ajili ya vifaranga kilogram 15 .
Baada ya apo utaendelea kuweka unga wa mifupa kilogram 5 kama ambavyo uliandaa katika maandalizi yetu, hakikisha umepima kilogram 5 bila kupunguza au kuzidisha.
Alafu utaendelea kuweka chokaa ambayo ni maalum kwaajili ya mifugo kilogram 9 1/4 bila kuongeza au kupunguza
Ukishaweka chokaa utaendelea kuweka chumvi iliyosagwa yani chumvi ilemaalum kwa ajili ya mifugo 1/2 (nusukilogram)
Alaf utamalizia kwa kuweka layer primix 1/4(robo kilo) (ndugu msomaji wangu mahitaji yote utayapata kwenye duka lolote la pembejeo za kilimo na mifugo)
Baada ya kuweka mahitaji yako yote kwenye sehemu uliyoiandaa utaanza kuchanganya ndugu kwenye kuchanganya unaweza kutumia beleshi (chepe) kwa kukichanganya mpaka uone mchanganyiko wako umeenea kila sehemu ukishachanganya hivyo chakula chako kitakuwa tayari kwaaji ya vifaranga wako. Ndugu msomaji unaweza pia uka tengeneza zaidi ya kilo mia moja cha kufanya ni wewe uongeze mahitaji kwa kadri utakavyokuwa unahitaji.. kwaleo naomba niishie hapo nakusihi uendelee kusoma mtandao huu kwani utakuwa unapata mambo mazuri kuhusu ufugaji, ndugu ukiwa na tatizo lolote tuwasiliane kupitia cm number +255744874288 asante.
Hakuna maoni: