jinsi ya kuanzisha mradi wa kuku


 Ndugu mfugaji mwenzangu, yafuatayo n mambo muhimu ya kuzingatia katika kuanzisha mradi wa kuku.


Ndugu iliupate kuku bora kwaajili ya uzalishaji wako lazima uchague jogoo  na migetea  walio bora.

Vitu vya kuzingatia wakati wa kununua kuku wa kufuga.

Kuku wazuri kwa ajili ya kuatamia na kutaga mayai mengi ni wale walio na umbo kubwa kwani wanapo tamia mayai wanakuwa na uwezo wa kuangua yote.
Chagua kuku ambao wanakua harama yaani ambao hawaja dumaa, kuku walio dumaa watakusumbua sana wakati wa utagaji kwani hawatagi mayai mengi wanaweza kutaga mayai nane na wakitaga mayai mengi watataga mayai kumi tuu.
Chagua kuku ambao wanastahimili magonjwa. Kuku wa kienyeji niwazuri sana kwa kustahimili magonjwa pia kuku chotara nao pia ni wazuri kwani hawashambuliwi na magonjwa sana.
Jogoo unao wachagua hakikisha hawana uhusiano wa damu na mitetea ulio wa chagua.
Pia unapo chagua jogoo na mitetea hakikisha kuwa umechagua jogoo kulingana na idadi ya mitetea,0 yaani jogoo mmoja kwa mitetea kumi au jogoo wawili kwa mitetea ishirini.

Sehemu ya kuatamia na kuangulia.

Kiota kizuri kwa ajili ya kuatamia ni kile ambacho umekiandaa kabla ya kuku kutaga, kiota kinatakiwa kiwe cha duara au unaweza kukitengeneza kama sahani baada ya kukiandaa pulizia uko dawa kwaajili ya kuuwa wadudu kama chawa, utitiri na viroboto.

Maandalizi kwaajili ya kuku anae taatamia.

Mkague kuku kabla hajaanza kuatamia ilikuhakikisha kuwa hana wadudu kama utitiri na chawa kwani hawa wanamsumbua sana wakati wa kuatamia.
Pia kuku akianza kuatamia mpechakula chakutosha iliaweze kuwa na joto jingi kwaajili ya kuangua mayai, ndugu kuku waliopewa chakula cha kutosha wanakuwa na uwezo wa kuangua mayai yote uliyo muwekea kwa wakati.
Kuku akianza kutaga kama wapo wengi akianza mmoja unaweza ukampa yai moja kwanza huku ukiwazubiria wengine waanze kuatamia lengo ni kuweza kupata vifaranga wengi kwa wakati mmoja. Pia kuku anae atamia anatakiwa apewe mayai kumi na matatu au kumi na mawili.
Ukifanya hivi kwa kuku kadhaa wanao taga kwa kipindi kifupi utakuwa na vifaranga wengi ambao watakuwa kwa kipindi kimoja tena kwa pamoja.

Hakuna maoni:

CHANGE LANGUAGE

Inaendeshwa na Blogger.