Ugonjwa Wa Coccidiosis
COCCIDIOSIS.
Ugonjwa huu husababishwa na protozoa.
Coccidiosis(kuhara damu)_ ugonjwa huu huonekana
katika sura mbili.
(1) Caecal coccidiosis ___Sura hii ya ugonjwa hushika
vifalanga.
Dalili zake
_Vifaranga huonekana wamezubaa, kushusha mabawa
_Kinyesi kuonesha damu
_Vifo vingi hutokea
_Vifaranga kushindwa kula na kunywa.
_Damu huonekana kwa wingi katika kinyesi kabla ya kifo.
Katika sura hii Kifaranga chenye coccidiosis sio lazima
kionesha dalili zote au kinyesi cha damu. Hapana unaweza
kuona Vifaranga wako wamezubaa , huku wameshusha
mabawa vifo vingi kila asubuhi unakuta vimekufa .
sipo kuwa makini unaweza kujiuliza ni ugonjwa gani?
Kwa kuwa umezoea mpaka uione damu kwenye kinyesi
ndio ujue kuwa ni coccidiosis.
(2)Intestinal coccidiosis__ Sura hii ya ugonjwa hushika
kuku wakubwa.
Dalili zake.
_Kuku kupunguza ulaji wa chakula
_Kuku kupungua uzito
_ Kuku kuangusha mabawa
_Kuku kuharisha kijivu na damu , ugoro na mala nyingi
kinyesi kuwa na damu damu
_ Kuku kukonda
_Utagaji wa mayai kupungua sana.
UKIUPASUA MZOGA
1 Utumbo kuonekana na damu
2Utumbo butu kuwa na damu damu
3Utumbo butu kuvimba
4Utumbo sehemu za ndani kuonekana kama vile
umesagika,cloaca ya kuku hubadilika rangi na kuwa navidotidot kama vya damu tunaita [hemorrhage]
KUZUIA UGONJWA HUU:
_ Epeka hali ya unyevu unyevu katika banda la kuku
_Ni muhimu kizingatia hali ya usafi kwenye banda la kuku
MATIBABU YA UGONJWA WA COCCIDIOSIS.
_Esb3
_Anticox
_Vitacox
_Amprolium
Hakuna maoni: