VISABABISHI AMBAVYO VINAWEZA KUCHANGIA KUKU WASITAGE VIZURI
Nawasalimu Nyote
Karibu Tuvijue Visababishi Ambavyo Vinaweza Kuchangia Kuku Wasitage Vizuri:-
1. Kuku wasipopewa chakula kwa wakati, chakutosha na bora (balanced diet).
2. Joto Likiwa Kali (Heat Stress). Hili huwapunguzia hamu ya kula na pia kuku hutumia nguvu nyingi kupambana kupunguza joto.
3. Kuku wasipopata mwanga wa jua na majani ya kutosha.
4. Minyooo. Minyoo hutumia sehemu kubwa ya chakula kinacholiwa na kuku hivyo kusababisha utagaji na ukujua kua duni.
5. Msongamano wa kuku bandani (Overcrowding).
6. Chakula Kuwa Na Protein Nyingi Ambayo Hufanya Miili Yao Kujaa Mafuta Inasababisha Wasitage pia.
7. Baridi huachangia kuku kupunguza kutaga vizuri kwasababu wanatumia nguvu nyingine kujikinga na baridi kwaiyo utagaji unakua sio mzuri.
8.Magonjwa mfano wa Typhoid, Ugonjwa wa kuhara damu (Coccidiosis) nk.
Tufanyeje Nini Kuzikabili Hizi Changemote
1. Kuku/ndege wapewe chakula chakutosha, kwa wakati na chenye viinilishe vyote muhimu(balanced diet).
2.Hakikisha Kuku wako wanapata chanjo zote muhimu na dawa za minyoo kila baada ya miezi 3.
3. Hakikisha Kuku wanapata mwanga wa kutosha na majani.
4. Kuku wapate nafasi ya kutosha bandani
Hakuna maoni: