Jinsi ya kulea vifaranga wa Bata mzinga



Vifaranga wa bata mzinga ni tofauti
na wa kuku kwani vifaranga wa
kuku hutotolewa wakiwa tayari
wanajua kujifunza kula na kunywa
maji wakati wale wa bata mzinga
huzubaa kwa siku kama 4 ndipo
wajue kula vizuri. Hivyo wana hitaji
uangalizi wa karibu na wa hali ya juu
sana.
Hukaa kwenye bruda (brooder) kwa
muda wa wiki 4 wakiwa watahitaji
joto la kutosha muda wote. Wiki ya
kwanza wanahitaji nyuzi joto 38 na
wiki ya pili unapunguza nyuzi joto 5
na kila wiki utaendelea kupunguza
nyuzi joto 5. Wanakua kwa haraka
hivyo wanahitaji sehemu kubwa ya
kuwatunzia, yaani sentimita 20×20
kwa kila kifaranga kwenye wiki ya
pili hadi ya tatu. Wanahitaji chakula
chenye protini nyingi 28% kwa wiki 8
za mwanzo, hivyo ni bora kuwapa
broiler starter kwa muda wa miezi
miwili.
Mambo muhimu ya kuzingatia kwenye
uleaji wa vifaranga vya bata
1. Hakikisha unaweka matandiko
(brooder) sehemu ya kuwalelea
vifaranga kiasi cha kutosha
(kina cha inchi 3) ili kuweka
hali ya joto. Matandiko yaweza
kuwa maranda ya mbao, nyasi
au pumba za mpunga.
2. Wape joto kwa vyanzo vya joto
ulivyo navyo kama taa za
umeme 100w au 200w, jiko la
mkaa, taa ya chemli au kandiri
au tumia njia za asili. Njia nzuri
na isio na gharama kubwa
yakutengeza joto ni
kwakutumia jiko la mkaa
liwashe nje likisha waka vizuri
liingize kwenye chumba chao.
Ni rahisi kutambua kama joto
linawatosheleza ama la. Joto
linapokua kali utawaona
vifaranga wakiachama midomo
kama vile afanyavyo mbwa pia
hutanua mbawa zao na
kuachiana nafasi. Ukiona hivyo
fungua madirisha kwa muda
mpaka wawe kwenye hali ya
kawaida kisha funga tena
madirisha ili kuhifadhi joto
kuokoa matumizi ya mkaa mara
kwa mara. Joto linapopungua
vifaranga hukusanyana hapo
tambua kwamba wanasikia
baridi hivyo ingiza jiko ndani.
Njia hii yakutumia jiko ni rahisi
kwani kama utawasha jiko
usiku saa mbili hutaweka tena
mpaka asubuhi cha msingi
chumba kisiwe na upotevu wa
joto.
3. Weka vyombo vya chakula na
kunywea maji kabla
hujawaingiza vifaranga hao.
4. Weka vitu vya kung’aa katika
chakula na maji ili kuwavutia
kujifunza kula. Vitu vya kung’aa
yaweza kuwa gololi zile za
kuchezea watoto unatumbukiza
kwenye maji hivyo zile rangi
zitawavutia kusogea pale na
kudonoa donoa. Au waweza
kuweka maji ya mchele kama
maji yao ya kunywa ili ile rangi
nyeupe iwavutie kusogelea
maji. Pia unaweza kuamua
kuwachanganya na vifaranga
wa kuku watajifunza kula
kupitia vifaranga wa kuku. Hii
ni namna ya kuwafunza kula.
5. Wape chakula muda wote na
wape majani wiki ya pili maana
asilimia 50 ya chakula chao ni
majani ya mbogamboga mbichi.
Chanjo na madawa
Chanjo: Kama ilivyo kwa kuku bata
mzinga wanahitaji dawa na chajo.
Wiki ya kwanza: Wape chanjo ya
Mdondo/kideri (Newcastle), Ndui
(Fowl pox) na Mbande (Gumboro).
Wiki ya sita: Rudia chanjo ya
Mdondo, kila baada ya miezi mitatu
Madawa: Madawa hasa antibiotic
pindi unapoona viranga vinaonesha
dalili za kuumwa na tatizo kubwa
kwa vifaranga ni ugonjwa wa
chorera (Magonjwa ya matumbo).
Magonjwa mengi ya matumbo
hutibiwa kwa antibiotic hasa OTC
20% pia ni vema ukafika kwa
mtaalumu wa mifugo kama uko
jirani ili upate matibabu sahihi kwa
bata wako.
Wape vitamini na madini ktk
chakula chao na vitamini nzuri ni ile
yenye mchanganyiko wa vitamini
nyingi (Multivitamin). Multivitamin
inaweza kutumika wakati wote
kwani husaidia kuwapa vifaranga
vitamini pia huviongezea nguvu.
Chakula: Ikifika wiki ya 8 unaweza
kuanza kuwatoa nje wajifunze
mazingira ya nje na kujitafutia
maana bata mzinga ni watafutaji
wazuri wa chakula kama kuku wa
kienyeji japo hupenda sana majani.
Ni vizuri kuwapa lusina mbichi
hufanya vizuri katika bata mzinga.
Wape vifaranga vyakula venye
mchanganyiko maalumu walau kwa
miezi miwili. Vyakula hivi vinauzwa
madukani lakini pia kama unaweza
na kuelewa mchanganyiko huo
unaweza fanya mwenyewe.
Utagaji wa mayai: Wiki ya 24 hadi 28
wanakuwa tayari wana kilo 8 hadi 12
hivyo wanaanza kutaga wachanganye
na maduma katika ratio ya 1:5 yani
dume 1 majike 5 hii ni kama bado
hawajawa wazito sana kama
wameshakuwa wazito au kuanza
kuwa wavivu kuzeeka wawekee ratio
ya 1:3 yani dume 1 majike 3.
Bata mzinga hutaga kwa msimu
kama walivyo kanga na hulalia siku
28 kama kanga na wanauwezo
wakulalia mayai yao 10 hadi 15 lakini
hutaga mengi zaidi hivyo ni vizuri
ukatumia mashine ya kutotolesha au
kama una kuku wa kienyeji anapo
lalia unamuwekea mayai 6 ya bata
mzinga. Hivyo wakati huo bata
anaendelea kutaga huku wanalalia
mayai yao. Hivyo ni njia nzuri maana
bata mzinga wanatabia ya kususa
mayai yao kama mtu ukiyashika na
marashi au yakipata harufu ambayo
sio yao.
Soko: Soko la bata mzinga lipo mpaka
sasa wanunuzi wanakuja kununua
shambani kwako kwa sh 12,000/=
kwa kilo moja ya bata mzinga na
bata mzinga wakubwa wana zaidi ya
kilo 15 kila mmoja.


JINSI YA KUTUNZA WATOTO WA BATA
MZINGA (TURKEY)



Kumekuwa na mawazo au kasumba
kwamba ufugaji wa bata mzinga,
hasa kukuza vifaranga ni mgumu
sana ukilinganisha na kuku. Ni kwa
nini? Baadhi ya watu huchukulia
bata mzinga kama vile kuku – hapa
nikimaanisha pindi anapototoa
unaweza kumuachia vifaranga na
akaweza kutembea navyo na
kuvikuza mwenyewe atakavyo – LA
HASHA! Bata mzinga ni mzembe kwa
kiasi Fulani katika kuangalia au
kutunza vifaranga wake hasa wakiwa
wadogo ukilinganisha na Kuku.
Hizi ni baadhi ya mbinu au taratibu
ninazozitumia kukuza vifaranga wa
bata mzinga.

1. MAYAI – Bata mzinga ana
uwezo wa kutaga mayai mengi
ili mradi uwe unayatoa mayai
pale anapotaga na kuyahifadhi.
Binafsi hutumia incubator
kutotoresha mayai ya Bata
Mzinga – lakini bata mzinga vile
vile ana uwezo wa kuatamia
mayai kati ya 15 mpaka 20
(inategemea na umbile lake).
Mayai yanapotagwa huyaifadhi
kwenye tray (sehemu ya wazi)
kwa muda wa siku 10-12
Maximum na kuyaweka kwenye
machine. Vifaranga huanguliwa
baada ya siku 28.

2. UTUNZAJI – Vifaranga hawa
huwa nawaweka kwenye
brooder maalumu ambayo
huhifandhi joto. Vifaranga wa
bata mzinga huhitaji joto la
kutosha hasa katika wiki ya
kwanza huhitaji nyuzi joto 95 –
100 (degrees) na unaweza
kuwapunguzia nyuzi joto 5 wiki
ya pili na kuendelea mpaka
watakapo ota manyoya kati ya
wiki 5-6. Hata wakiota manyoya
ni vizuri kuendela kuwawekea
taa ya mwanga wa kawaida
hasa wakati wa usiku ndio
muda ambao wanapenda
kupata chakula na kucheza.
3. CHAKULA – Vifanga wa bata
mzinga hupendelea chakula
chenye PROTEIN kwa wingi
ukilinganisha na Kuku. Katika
mchanganyiko wa Chakula
kiwango cha virutubisho vya
Protein ninachoweka ni asilimia
ishirini na nane (28%). Mara
nyingi mimi natumia unga wa
samaki aina ya FURU au dagaa
au UDUVI (hawa ni worms
ambao huvuliwa pamoja na
dagaa – ziwa Victoria) – kama
sehemu ya Protein. Kwa ujumla
chakula cha vifaranga wa Bata
mzinga (Starter) kinatakiwa
kiwe chenye muonekano wa
unga unga (punje ndogo ndogo
sana) ili kisiwakwame kooni
wanapokula. Chakula
kinapowakwama utengeneza
madonda kooni hivyo kifaranga
hudhoofika kwa kuacha kula. Ni
vizuri vile vile kuchanganya
vifaranga wa bata mzinga na
wa kuku ili waweze
kuwachangamsha hasa wakati
wa kula chakula.
4. MAGONJWA – Kama hautakuwa
makini kwa kuzingatia joto hasa
wiki ya kwanza – Vifaranga wa
bata mzinga hushambuliwa na
ugonjwa wa Nimonia na
huathiri mfumo wa kupumua
na hatimaye kifo. Magonjwa
kama concidiocise, fow cholera,
ndui (fow pox) n.k
huwashambulia sana vifanga
wa bata mzinga.
5. KINGA/TIBA – Baada ya siku 7
vifaranga wa bata mzinga
wapewe chanjo ya kinga ya
kideri na wiki inayofuata
wapewe chanjo ya Gumboro.
Baada ya wiki ya 5 wapewe
chanjo ya kinga ya Ndui. Vile
vile mimi hutumia dawa za asili
hasa vitunguu swaumu kwa ajili
ya kinga ya Mangonjwa kuanzia
wiki ya kwanza mpaka ya tano
huwawekea vitunguu swaumu
kwenye maji ya kunywa
nikichanganya na vitamin – hii
husaidia sana kuwapa kinga ya
bacteria wanaoweza
kushambulia miili ya vifaranga
hao.
Image result for BATA MZINGA

Hakuna maoni:

CHANGE LANGUAGE

Inaendeshwa na Blogger.