FAHAMU VYAKULA VINAVOTUMIKA KUNENEPESHA NGURUWE



Mahitaji ya muhimu katika kuandaa chakula cha kunenepesha nguruwe.

Mahindi yaliyo sagwa au unga wa mahindi kilo ishirini na tano 25kg, pumba ya mahindi kilo hamsini na tano 55kg, mashudu ya alizeti kilo kumi na nne 14kg, dagaa walio zagwa kilo tatu 3kg, chokaa ya mifugo kilo mbili 2kg, pig mix 0.5kg (1/2kg) na  na chumvi iliyosagwa nusu kilo.
Hayo ndio mahitaji ya muhimu katika uandaaji wa chakula cha kunenepeshea nguruwe.
Kumbuka kuwa chakula hiki ni kwaajili ya kunenepeshea nguruwe tuu kamwe usikitumiekwa ajili ya ngombe au mbuzi kwani kwa ngombe na mbuzi huwa wanatumia chakula chao chatofauti na nguruwe.
Wala usitumie kwaajili ya kuku endapo utatumia kwaajili ya kuku kitasababisha kuku kudumaa.
Pia ndugu chakula hiki ukikitumia kwa muda wa miezi miwili bila kuchanganya na kitu kingine nguruwe wako watanenepa sana na utaweza kutengeneza hela nnzuri sana  kwa muda mfupi.

Hakuna maoni:

CHANGE LANGUAGE

Inaendeshwa na Blogger.