Changamoto Za Ufugaji Kuku
.
Leo nazungumzia changamoto ya shughuli nzima ya ufugaji wa kuku.
Najua watu wengi wamekimbilia kwenye sekta hii kutokana na jinsi makala kuhusiana na faida za ufugaji kuku na utajiri uliopo kwenye shughuli hii huonekana ina faida kubwa sana lakini makala nyingi huishia kwenye faida magonjwa, chanjo na jinsi ya kujenga mabanda, tuachane na hayo turudi kwenye mada zifatazo ni changamoto za shughuli hii ya ufugaji kuku:
MTAJI MKUBWA WA KUANZISHA SHUGHULI HII
Mtaji wa kuanzisha shughuli hii ni mkubwa ukilinganisha na makadirio wanayoyaweka katika makala nyingi za ufugaji wa kuku, mtaji wa kianzio hutumika kufanya yafuatayo:
1.Gharama za mafunzo na miongozo ya ufugaji huu mf video, vitabu, Ada za Semina na nauli za safari kuangalia wakulima waliofanikiwa katika sekta hii ya ufugaji wa kuku,
2.Gharama ya kufanya utafiti wa soko la bidhaa zako mf mayai, nyama, mbolea.
3.Kununua/kukodi eneo kwa ajili ya shughuli hii
4.Ujenzi wa mabanda, fensi.
5.Kuweka miundo mbinu muhimu kama maji na umeme
6.Mshahara wa wafanya kazi
7.Ununuzi wa vifaranga
8.Chanjo,madawa ya kuua wadudu
9.Mavazi Maalum ya kazi hii
10.Vyombo vya maji/chakula
11. Vyakula vya kuku n.k
MILIPUKO YA MAGONJWA
Wafugaji wengi wamepoteza kuku wengi kutokana na magonjwa wengine wamekata tamaa na kuiacha shughuli hii magonjwa hayo ni kama kideri, mdondo, mafua, kifua kikuu cha kuku n.k.
Mengi katika magonjwa hayo yametokana na kutofuga kitaalam,uzembe wa wafanyakazi, uchafu, mabadiliko ya hali ya hewa.
BEI KUBWA YA VYAKULA VYA KUKU
Hii ni changamoto nyingine ambayo imewakumba na inaendelea kuwatesa wafugaji wa kuku kumekuwa na wimbi kubwa la wazalishaji wa vyakula vya kuku lakini bei ya vyakula hivyo haina uhakika leo utakuta bei hii kesho bei nyingine mamlaka zinazohusika zimeshindwa kuweka bei elekezi kama Ilivyo kwenye bidhaa kama mafuta.
WAFANYAKAZI KUTOKUWA WAAMINIFU
hii ni changamoto nyingine inayowakumba wafugaji wa kuku wengi kwani vijana wa kazi wengi sio waaminifu
kwani ukishindwa kusimamia vizuri mradi wako hautadumu hata kidogo vijana hawa wamekua wakiuza vyakula vya kuku, mayai na kuku kama utakuwa mtu wa kuendesha mradi huu kwa kutumia simu bila kufika kwenye mradi wako.
UPATIKANAJI WA CHANJO HALISI
wafugaji wengi wamekua wakilalamika juu ya kupoteza kuku, vifaranga, kutokana na kukosa chanjo au kuchanja vifaranga/kuku chanjo bandia na wengi wanasumbuliwa na magonjwa mengi kutokana na kutumia chanjo bandia au kukosa chanjo sahihi kwa ajili ya kuku/vifaranga.
KUKOSA USHIRIKIANO KUTOKA SERIKALINI
Serikali haijalipa kipaumbele sekta hii hivyo kufanya wakulima wengi kukosa chombo husika unayoweza kuzalisha vifaranga bora, kuweka bei elekezi kwenye vyakula na kuweka chombo maalum kwa ajili ya kupima ubora
wa vyakula vya kuku, chanjo, kujenga vyuo vitakavyotoa mafunzo ya ufugaji wa kuku
SOKO LA UHAKIKA
hili limekua ni wimbo kwa wafugaji wa kuku wengi kwani wengi wamekosa ni wapi pakuuzia bidhaa zao hivyo kujikuta wakizalisha sana lakini hawana uhakika wa soko la la mayai, nyama.
BEI YA BIDHAA ZITOKANAZO NA SHUGHULI HII
Kumekua na tatizo katika bei za kuuza bidhaa hizi kwani bei hizo haziendani na gharama za uendeshaji wa miradi wafugaji wa kuku wengi wamepata hasara kutokana na jinsi bei ya bidhaa zao kua chini kuunganisha na gharama za uanzishaji na uendeshaji wa shughuli hii.
Hakuna maoni: