AINA MBALIMBALI ZA MAGONJWA YA KUKU NA TIBA ZAKE.

Magonjwa ya kuku, Tiba na Kinga

1) Ugonjwa wa Mdondo
Ugonjwa huu huathiri kuku katika umri wowote na
unapoingia kwenye kundi huweza kuua idadi kubwa ya
kuku hao hadi kufikia asilimia tisini. Ndege wakubwa
hustahimili kidogo kuliko wale wadogo kwasababu ya
usugu mwilini (body immunity) uliojengeka kwa muda
mrefu zaidi.
Ugonjwa huu husababishwa na kimelea cha kirusi
kiitwacho Paramyxo viridae na huenezwa kwa njia ya
hewa na kugusana.
Dalili zake :
Kukohoa na kuhema kwa shida
Ute hutoka mdomoni na puani
Kuku walioathirika hupata kizunguzungu.
Kuharisha uharo wa kijani na njano
Kuzubaa, kusinzia na mabawa kushuka
Baada ya siku 2 kuku hupindisha shingo
Kuvimba macho
Kuzunguka
Kuku hutaga mayai hafifu.
90% ya kuku huweza kufa
Tiba:
Ugonjwa huu hauna dawa.
Kinga:
Kuchanja;
Chanja kuku wako kila baada ya miezi mitatu /na
mara nne kwa mwaka.
Kuna chanjo aina mbili za ugonjwa huu, nazo ni;
1. Lasota:
Chanjo hii hutolewa katika dawa yenye umbile la
kidonge kimoja kimoja ambacho kina dozi ya kuku
1000 na huwekwa kwenye maji ili kuku wanywe hiyo
dawa.
Inashauriwa kuku wanaopewa dawa hii wanyimwe maji
ya kunywa siku moja kabla yake
Ni  vizuri kuwapa mchanganyiko maalum wa dawa
wenye mchanganyiko wa  vitamin na dawa ya
kuwaongezea kuku nguvu. Dawa hii itolewe saa moja
au zaidi  baada ya kuwapa chanjo ya mdondo.
Thermostable I NCD vaccine :
o   Huwekwa katika chupa kimoja (vial) chenye dozi
400 za kuku
o   Chanjo hii inavumilia joto ikikaa bils nje ya jokofu
kwa muda mrefu zaidi.
o   Imetengenezwa katika mazingira ya nchi za joto.
Na inaweza kukaa kwa siku 14-15 ikiwa itatunzwa
ipasavyo hata baada ya kutumia mara ya kwanza.
2) Kuharisha Damu (Coccidiosis):
Ugonjwa huu husababishwa na kimelea cha protozoa
cha jamii ya Eimeria (Eimeria tenela , Eimeria maxima ,
na Eimeria acervulina )
Kwa kawaida wadudu hawa hupenda kuishi kwenye
mazingira machafu, kama vinyesi, vyakula vilivyooza
na umaji maji (moist environments).
Dalili zake :
Kinyesi chake huchanganyika na damu
1)      Wakati mwingine kuku hunya damu
2)      Kuku hudhoofika sana
3)      Kuku huteremsha mabawa yake
4)      Hatimaye vifo hutokea
Tiba;
Ugonjwa huu hutibika kwa kutumia dawa za
(i) Kundi la suphur
Mfano: sulphonamides (ESB3) kwa siku 3-4
(ii) Amprolium
Dawa za ugonjwa huu hupatikana madukani hivyo
ukipatwa na tatizo hilo fika kwenye maduka ya dawa
aua muone mganga wa mifugo.
Kinga:
Zingatia usafi mara kwa mara
Kwakuwa ugonjwa huu huambatana na majimaji na
uchafu wenye vimelea vya ugonjwa huu, ni  vizuri
kuhakikisha banda la kuku linakuwa safi na kavu
wakati wote.
Tenga kuku wagonjwa kutoka kwa walio wazima.
Tumia dawa ya kinga ili kuepusha uwezekano wa
kuku kuambukizwa ugonjwa huu
Dawa inayopendekezwa ni zile zinzoitwa (coccidiostat.
Tenga kuku wadogo (vifaranga) kutoka kwenye
kundi la wakubwa.
3) Homa ya Matumbo (fowl typhoid)
Husababishwa na vimelea vya wadudu wa bakteria wa
jamii ya Salmonella.
Kimelea hicho cha bacteria
huitwa Salmonella gallinarum.
Dalili zake :
Uharo mweupe au wa kijani
Vifo hufikia kiasi cha 50%
Rangi ya minofu hugeuka kuwa ya njano
Viungo vya ndani kama maini , figo , bandama
huvimba
Maini hung’aa kwenye mwanga mkali.
Tiba :
Tumia dawa za antibiotiki kama vile furazolidone ili
kutibu ugonjwa huu.
KINGA: Chanja kuku wako mara kwa mara .
Fanya usafi wa banda na vyombo vya kulishia na
kunyweshea maji ipasavyo.
4) Ugonjwa wa Mafua ya Ndege
Ugonjwa wa mafua ya ndege ni ugonjwa hatari
sana kwa kuku na jamii nyingine za ndege.
Pia ugonjwa huweza kuambukizwa na
kusababisha vifo kwa binadamu.
Ugonjwa huu husababishwa na kirusi
kiitwacho Orthomyxo virus .
Ugonjwa huu huenezwa kwa njia ya kugusana
baina ya ndege na ndege  na baina ya ndege na
binadamu.
Dalili zake
Dalili za ugonjwa huu huanza kuonekana katika kipindi
cha siku 3-7 baada ya kuku kuambukizwa.
Dalili hutofautiana kutokana na umri wa ndege.
Baadhi ya dalili zake nihizi zifuatazo
Kuku /ndege hupumua kwa shida (dyspnoea).
Kuzubaa.
Kutokwa na machozi.
Kukohoa na kupiga chafya.
Kuharisha kinyesi chenye majimaji.
Sehemu za kichwa zisizo na manyoya
huvimba.uvimbe wenye majimaji huonekana
kichwani na shingoni.
Sehemu ya juu kichwani hubadilika na kuwa na
rangi ya bluu iliyopauka.
Kuku hutaga mayai yenye maganda laini.
Tiba:
Ugonjwa huu hauna tiba .
Kinga na kuzuia kuenea kwa ugonjwa huu:
Toa taarifa kwa mganga (daktari wa mifugo
aliye karibu ukiona dalili za ugonjwa huu.
Tenga mabanda ya kuku wagonjwa na walio
wazima.
Fungia kuku wako wasitembee holela.
Acha kununua kuku kutoka eneo linalohisiwa
kuwa na ugonjwa huu.
Acha kusafirisha mifugo /ndege bila idhini ya
daktari.
Zuia wageni kutembelea mabanda yako ya kuku.
Acha kuhamisha mbolea ya kuku kwenda
shambani kutoka kwenye banda la kuku
wanaoumwa ugonjwa huu.
Safisha mabanda na kuweka dawa chini ya
usimamizi wa mtaalamu wa mifugo na
kulipumzisha kwa siku 21kabla ya kuanza kufuga
tena.
Choma moto mkali au fukia chini mbolea kutoka
kwenye banda la kuku wanaoumwa ugonjwa huu.
Pata ushauri kutoka kwa mtaalamu wa mifugo
aliye karibu nawe.
5) Gumboro (infectious Bursal Disease)
Ugonjwa  huu husababishwa na kirusi
Dalili zake:
o   Hushambulia vifaranga
o   Uharo mweupe
o   Kuchafuka (dirting of anal area)
o   Kuvimba
o   Kiwango kikubwa cha vifo
o   Damu hutapakaa eneo la kutolea kinyesi
Kinga:
1)      Usafi
2)      lishe bora
3)      chanja vifaranga wakiwa na umri wa wiki
tatu  kwa kutumia chanjo hai (live vaccine)
6) Kifua Kikuu cha Ndege(Avian Tuberculosis-TB)
Husababishwa na kimelea
aitwaye Mycobacterium avium.
Dalili zake:
o   Kukonda na Kupungua uzito
o   Vidonda  kwenye kishungi
o   Kupungua uzito/kukonda
o   Kuhara
Kinga:
Usafi:
Fanya usafi na vyombo , banda na mazingira .
7) Magonjwa yatokanayo na Lishe (Nutritional and
Metabolic Disorders)
Dalili za magonjwa haya hutegemea aina ya
virutubisho vinavyokosekana mwilini
Kwa mfano:
o   Kupinda miguu (rickets) husababishwa na upungufu
wa Vit.D, madini ya calcium na fosforasi.
o   Vidonda vyenye vyenye damu husababishwa na vit.K
o   Kichaa cha kuku na kusinyaa kwa misuli
husababishwa na upungufu wa Vit.E
o   Magamba ya Mayai (egg shell)kuwa laini  ama umbo
kuwa  bovu husababishwa na upungufu wa madini ya
calcium na fosforasi.
o   Kudonoana kusababishwa kwa njia moja au
nyingine na upungufu wa chakula na madini ya
fosforasi na calcium
o   Kuvimba macho, upungufu wa damu huletwa na
upungufu wa vit.A.
Kinga:
o   Kuwapa kuku mlo kamili
o   Kuelewa kwa kina aina za chakula kwa kila rika na
aina ya kuku ; vifaranga , kuku wa mayai na wa
nyama. (Poultry age and classes i.e chicks, layers and
broilers)
o   Kufanya uchunguzi wa virutubisho vilivyomo katika
aina ya chakula unachotumia.
8) Minyoo (Helminthiasis)
Minyoo iko ya aina tatu kama vile minyoo kamba,
minyoo bapa na minyoo ya mviringo
Dalili zake:
Kudumaa
Kuwa manyoya hafifu
Kupungua uzito
Kukonda
Minyoo huonekana kwenye kinyesi
Kinga /kuzuia:
USAFI:
Fanya usafi wa vyombo, banda na mazingira.
Tenga vifaranga kutoka kwa wale wakubwa.
Badilisha matandazo kuondoa mazalia ya minyoo.
Badilisha matandazo kila baada ya miezi mitatu.
Tiba:
Tumia dawa zinazopendekezwa na wataalamu
hasa zile zinazoua minyoo ya aina zote (mfano:
piperazine citrate).
Hakikisha kila baada ya miezi mitatu unawapa
kuku wako dawa za minyoo.
9) Kupe, Utitiri, Chawa na Viroboto
kupe laini  waitwao Argus persicus, chawa na viroboto
wanaong’ata .
Dalili zake:
Kujikung’uta.
Kupiga kelele.
Kiasi cha damu hupungua mwilini.
Utando wa ngozi ndani ya kope za macho
hupauka.
Utando wa ngozi ya juu mwilini huwa mnene.
Magamba ya unga-unga hudondoka.
Kuzuia:
Tupa au choma masalia ya mayai yasiyoanguliwa
na magamba ya mayai yaliyoanguliwa vifaranga.
Safisha banda mara kwa mara na kunyunyizia dawa;
kuna dawa zinazopendekezwa na wataalamu za
kunyunyizia kwenye banda la kuku. Mfano wa hizo
dawa ni sevin , akheri powder n.k (Dawa hizi ni za
unga).

Usisahau Ku like facebook page yetu ili usipitwe na somo lolote lile.

Hakuna maoni:

CHANGE LANGUAGE

Inaendeshwa na Blogger.